Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 21, 2024 Local time: 09:21

Ufisadi wajikita katika sekta ya miundombinu ukizorotesha maendeleo Malawi


Mwandishi wa habari za uchunguzi Gregory Gondwe, picha iliyotolewa kutoka katika kurasa ya Facebook, aliiambia VOA Feb. 2, 2024, kuwa amekwenda mafichoni baada ya kuchapisha habari iliyokuwa inaanika vitendo vya ufisadi katika Jeshi la Ulinzi la Malawi.
Mwandishi wa habari za uchunguzi Gregory Gondwe, picha iliyotolewa kutoka katika kurasa ya Facebook, aliiambia VOA Feb. 2, 2024, kuwa amekwenda mafichoni baada ya kuchapisha habari iliyokuwa inaanika vitendo vya ufisadi katika Jeshi la Ulinzi la Malawi.

Sekta za Uchumi na uwajibikaji nchini Malawi vinaisihi serikali kushughulikia dosari katika mfumo wa ununuzi wa umma.

Ripoti ya ajenda ya Malawi ya 2021 kuhusu Miradi ya Miundombinu ya Umma inaelezea jinsi rushwa ilivyokithiri katika sekta ya umma ya Malawi. Sekta ya ujenzi ikiathiriwa zaidi.

Bango linalowaonya waendeshaji magari kuhusu mashimo yaliyopo kiasi cha kilomita mia moja na mbili au zaidi na hii ni kwenye barabara ya M1 Malawi inayounganisha sehemu za kaskazini, kati na kusini mwa nchi.

Hii ni dalili tosha ya hali ya sasa ya miundombinu ya barabara. Wataalamu wa masuala ya kijamii na kiuchumi wameihimiza serikali kukarabati miundombinu ikiwa Malawi inataka kuimarisha maendeleo yake ya kiuchumi ya kijamii.

Barabara Mbovu na Mashimo

Barabara mbovu na mashimo ni sehemu muhimu ya uzoefu wa wa kila siku mijini.

Licha ya kuwa tishio kubwa kwa madereva na abiria wao, wanawakilisha moja ya vikwazo vikuu kwa maendeleo ya uchumi wa kijamii ya nchi.

Jack Gama, mkaazi wa Lilongwe anaeleza: “Hali ya sasa ya barabara inazidisha gharama kwa magari, muda wa usafiri na pia ni changamoto kwa mizigo inayobebwa.”

Kutokana na hali ya barabara kuwa mbaya, madereva wa magari huchukua saa tatu kusafiri kati ya Lilongwe na Kasungu. Umbali ambao hapo awali humchukua mtu chini ya masaa mawili.

Mchumi Bertha Phiri anasisitiza kwamba miundombinu ya barabara nchini imeathiri ukuaji wa uchumi.

Mtandao wa Haki ya Kiuchumi

Bertha Phiri, Mkurugenzi Mtendaji Mtandao wa Haki ya Kiuchumi ya Malawi anasema:"Iwapo tutakuwa na miundombinu bora ya barabara, kitakachofanyika ni , kutakuwa na maendeleo ya kiuchumi na jamii yanayoweza kustawi kwa urahisi zaidi, kwa sababu barabara zina uwezo wa kuchochea kiwango cha biashara, kufungua masoko mapya, na kuvutia wawekezaji wapya."

Mashirika ya uwajibikaji na uwazi yanabainisha doari zilizopo katika mifumo ya ununuzi wa umma unaotoa fursa ya utoaji hongo, kuruhusu makampuni ya ujenzi ambayo hayajahitimu kupata kandarasi kuu.

Willy Kambwandira, Mkurugenzi Mtendaji Kituo cha Uwajibikaji na Uwazi kwa Jamii anaeleza:

“Tuna kandarasi zinazotolewa kwa watu binafsi ambao hawana hata mashine moja, wala kampuni. Tumeona pia miradi ya miundombinu isiyokidhi viwango kwa sababu kulikuwa na ushirikiano kati ya maafisa wa serikali na wakandarasi na kusababisha miradi mibovu ya miundombinu kutekelezwa.”

Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi

Katika kukabiliana na wasiwasi unaoongezeka kuhusu hali ya barabara nchini humo, Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi, Jacob Hara, amewahakikishia Wamalawi kuhusu juhudi za kufanya marekebisho ya haraka.

Kutokana na hali hii, mdhibiti wa sekta ya ujenzi, Baraza la taifa la Sekta ya Ujenzi la Malawi (NCIC) limejitahidi na kuweka usimamizi dhabiti kwenye miradi iliyopo.

Gerald Khonje, Mkurugenzi Mtendaji Baraza la Kitaifa la Sekta ya Ujenzi la Malawi anasema:

“Kuna mazingira ambayo yanasababisha miundombinu kuwa duni, mojawapo ikiwa ni rushwa. Baadhi ya miradi imeshindwa kutekelezwa tangu ilipoanzishwa. Njia ambayo mradi ulitumika kuanzisha mradi tayari unashindwa; wakati mwingine wanashindwa kufanya manunuzi.”

Sheria ya Taifa ya Sekta ya Ujenzi

Mdhibiti wa sekta hiyo aidha ametoa amri za kusitisha miradi ya ujenzi ambayo imekiuka makubaliano ya kimkataba kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Sekta ya Ujenzi.

Wasafiri wanasema hatua za haraka zinahitajika kurekebisha miundombinu na kuhakikisha utekelezaji wa matarajio ya nchi. Malawi inatazamia kuunda mfumo wa usafiri wa njia nyingi ifikapo mwaka 2063. Moja ya vipengele muhimu vya mpango huo ni kuwa na barabara zilizotunzwa vyema na zilizoboreshwa zinazounganisha maeneo ya mijini na vijijini.

Thom Khanje, Meneja Uhusiano wa Umma na Mawasiliano Tume ya Taifa ya Mipango anasema: “Tunaamini kwamba katika miaka michache ijayo, tutaona maendeleo, hasa katika miradi mikubwa kama vile barabara, ambayo haichukui miezi au hata mwaka kukamilika. Hii ni kwa sababu tumeshuhudia dhamira kubwa kutoka kwa serikali, sekta binafsi na washirika wa maendeleo.”

Ripoti ya kuhusu Sekta ya Miundombinu ya Benki ya Dunia ya mwaka 2023 inaonyesha kuwa Malawi inahitaji kwacha trilioni 1.5, sawia na dola milioni 8.6 kwa ajili ya miradi ya barabara ifikapo 2025 ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Forum

XS
SM
MD
LG