Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:27

Aliyekuwa spika wa bunge Afrika kusini ashtakiwa kwa tuhuma za ufisadi


Aliyekuwa spika wa bunge Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula akiwa mahakamani huko Pretoria. Aprili 4, 2024. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Aliyekuwa spika wa bunge Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula akiwa mahakamani huko Pretoria. Aprili 4, 2024. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ambaye alijiuzulu wadhifa wa uspika Jumatano, alifikishwa mahakamani mjini Pretoria baada ya kufika polisi na kukamatwa rasmi.

“Mashtaka dhidi ya Bi Mapisa-Nqakula ni makosa 12 ya rushwa na moja la biashara haramu ya fedha,” Bheki Manyathi wa Mamlaka ya Taifa ya Kuendesha Mashtaka ameiambia mahakama.

Akiwa amevaa nguo ya manjano na bluu iliyofanana na kitambaa chake cha kichwani alikaa kizimbani, mwanasiasa huyo mkongwe wa ANC alikaa kimya. Mahakama imekubali ombi la wakili wake kutaka aachiliwe kwa dhamana.

Hili likitokea chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi wa taifa, kesi imeongeza wasi wasi kwa ANC, ambayo inajitahidi kujiweka vizuri katika ukusanyaji maoni huku uchumi dhaifu na shutuma za rushwa kwa afisa na utawala mbaya.

Mapisa-Nqakula ni mmoja wa mwanasiasa mwandamizi wa karibuni wa ANC, akiwa pamoja na rais na makamu wa rais, kukumbwa na kashfa za rushwa.

Forum

XS
SM
MD
LG