Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 05:24

ANC inadai haitaki ushirikiano na chama kingine ili kushinda uchaguzi Afrika Kusini


Rais wa chama tawala cha ANC, Cyril Ramaphosa akihutubia wafuasi wake huko Soweto Septemba 3, 2023.
Rais wa chama tawala cha ANC, Cyril Ramaphosa akihutubia wafuasi wake huko Soweto Septemba 3, 2023.

Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC kinasema kina uhakika kitaendelea kuwa na wingi wa viti kwenye bunge la taifa wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Mai na kwamba hakijaanza mazungumzo na chama kingine cha kisiasa juu ya uwezekano wa kuunda serikali ya mungano.

Naibu katibu mkuu wa chama hicho Nomvula Mokonyane, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba "hatutakwenda vitani tukiwa na dhana ya kushindwa," aliongeza kusema "tuko vitani ili kupata ushindi."

Waafrika Kusini wanatarajiwa kupiga kura tarehe 29 Mei, ili kulichagua bunge ambalo hapo tena limamteuwa rais mpya.

Uchunguzi wa maoni unaonesha kwamba chama cha ANC kinaweza kupoteza wingi wake kwenye bunge kutokana na matatizo ya ulajirushwa, hali mbaya ya uchumi, ukosefu wa ajira na kashfa za mara kwa mara dhidi ya maafisa wa chama tawala cha ANC.

Chama kikuu cha upinzani Demokratik party kimeungana na vyama vingine vidogo katika juhudi za kukishinda chama cha ANC kwenye uchaguzi huo.

Forum

XS
SM
MD
LG