Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 04:06

Chama cha upinzani Afrika Kusini chavutia umati mkubwa katika kampeni za uchaguzi


Wafuasi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) wakihudhulia uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho huko Durban Machi 10, 2024. (Picha na RAJESH JANTILAL / AFP.
Wafuasi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) wakihudhulia uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa chama hicho huko Durban Machi 10, 2024. (Picha na RAJESH JANTILAL / AFP.

Chama cha upinzani cha Inkatha Freedom Party nchini Afrika Kusini kilikusanya umati mkubwa wa wafuasi kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mkuu na kujaza uwanja katikati ya ya makao yake ya Wazulu.

Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban ulikuwa umejaa kumsikiliza kiongozi wa chama Velenkosini Hlabisa akizindua ajenda ya IFP, lakini onyesho la kuvutia la nguvu siku ya kwanza linaweza kuwa kitovu cha kampeni kwa vuguvugu hilo.

Akitangaza kupitia hotuba yake ndefu, Hlabisa amesema Afrika Kusini inaelekea ukingoni mwa kuanguka, si kwa sababu ya ukosefu wowote wa watu lakini kwa sababu Afrika Kusini imekuwa chini ya utawala mbovu, uongozi dhaifu na ufisadi.

Uchaguzi wa Mei 29 utakuwa wa kwanza kupigwa na chama cha mrengo wa kulia bila mwanzilishi wake mashuhuri na kiongozi wa zamani Mangosuthu Buthulezi. Na sasa, inakabiliwa na changamoto mpya hata katika jimbo lake la KwaZulu-Natal (KZN), ngome muhimu ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG