Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 03:46

Upinzani wa Inkatha Freedom Party cha Afrika kusini kimezindua kampeni zake


Kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) Velenkosini Hlabisa akizungumza na wafuasi wake mjini Durban. March 10, 2024. (Photo by RAJESH JANTILAL / AFP)
Kiongozi wa chama cha Inkatha Freedom Party (IFP) Velenkosini Hlabisa akizungumza na wafuasi wake mjini Durban. March 10, 2024. (Photo by RAJESH JANTILAL / AFP)

Afrika Kusini iko ukingoni kuanguka sio kwa sababu ya ukosefu kwa watu wetu lakini kwa kuwa imekabiliwa na utawala duni na ufisadi

Chama cha upinzani cha Inkatha Freedom Party nchini Afrika Kusini kiliukutanisha umati mkubwa wa wafuasi wake kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zake za uchaguzi mkuu leo Jumapili, na kujaza uwanja katika eneo la makao yake ya Zulu.

Uwanja wa Moses Mabhida mjini Durban ulijaa kumsikiliza kiongozi wa chama hicho, Velenkosini Hlabisa akizindua ilani ya IFP, lakini kitendo cha kuonyesha umati mkubwa wa wafuasi katika siku ya kwanza kimedhihirisha kuwa kampeni hizo za chama zipo juu.

Afrika Kusini iko ukingoni kuanguka, sio kwa sababu ya ukosefu wowote kwa watu wetu lakini kwa sababu Afrika Kusini imekabiliwa na utawala duni, uongozi dhaifu na ufisadi, Hlabisa alisema katika hotuba ndefu.

Katika mwaka 2024 kwa urefu na upana wa Afrika, kuna wito mmoja wa kuhamasishana; wito wa mabadiliko. Uchaguzi wa Mei 29 utakuwa wa kwanza kupigwa vita na chama cha mrengo wa kulia bila mwanzilishi wake, na kiongozi wa zamani Mangosuthu Buthelezi na kinakabiliwa na changamoto mpya hata katika jimbo lake la nyumbani KwaZulu-Natal (KZN), eneo muhimu la mapambano ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG