Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 14:38

Afrika Kusini kufanya uchaguzi mkuu Mei 29


Rais wa Chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwahutubia wafuasi wake katika uwanja wa Dobsonville huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.
Rais wa Chama tawala cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa akiwahutubia wafuasi wake katika uwanja wa Dobsonville huko Soweto Septemba 3, 2023. Picha na Phill Magakoe / AFP.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza siku ya Jumatano kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo utafanyika Mei 29.

“Mbali ya kutekeleza wajibu wetu wa kikatiba, uchaguzi ujao pia unasheherekea safari yetu ya kidemokrasia na azma ya siku zijazo ambazo wote tunatamani” Rais Ramaphosa alisema katika taarifa.

Chama cha Ramaphosa cha African National Congess, ambacho kimetawala Afrika Kusini tangu uchaguzi wa kwanza wa baada ya enzi ya utawala wa kibaguzi mwaka 1994, kwa mara ya kwanza kiko hatarini kupoteza viti vyake vingi vya ubunge.

Ukusanyaji maoni kadhaa ya wapiga kura unaonyesha kuwa chama cha ANC kinaidhinishwa kwa kiwagno cha chini ya asilimia 50.

Chama cha ANC kwa miaka mingi kimegubikwa na matatizo na utata, ikiwemo kupanda kwa uhalifu, idadi kubwa ya ukosefu wa ajira, matatizo ya umeme ambayo yamesababisha kukatika kwa umeme, na shutuma za rushwa kuanzia wakati wa urais wa Jacob Zuma, kiongozi aliyekuwa madarakani kabla ya Ramaphosa.

Wapinzani wakubwa wa ANC, ni Democratic Alliance ambacho kimekuwa kikijaribu kujenga muungano wa vyama vidogo kupunguza wingi wa ANC, na chama cha mrengo wa kushoto cha Economic Freedom Fighters.

Chama ambacho kitashinda wingi wa viti katika bunge lenye viti 400, vitamchagua rais. Ramaphosa anagombea muhula wa pili wa miaka mitano ya mwisho.

Forum

XS
SM
MD
LG