Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:11

Marekani yawawekea vikwazo maafisa wa zamani wa serikali ya Malawi

PICHA YA MAKTABA: Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
PICHA YA MAKTABA: Rais wa Malawi Lazarus Chakwera

Marekani imewazuia maafisa wanne wa zamani wa serikali ya Malawi kuingia nchini,  kwa sababu ya kuhusika kwao katika ufisadi mkubwa, Wizara ya Mambo ya Nje ilisema Jumatano.

Marekani imewazuia maafisa wanne wa zamani wa serikali ya Malawi kuingia nchini, kwa sababu ya kuhusika kwao katika ufisadi mkubwa, Wizara ya Mambo ya Nje ilisema Jumatano.

Viongozi hao ni aliyekuwa mwanasheria mkuu na katibu wa sheria Reyneck Matemba, mkurugenzi wa zamani wa manunuzi ya umma na utwaji wa mali, John Suzi-Banda, aliyekuwa wakili wa polisi wa Malawi Mwabi Kaluba, na aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Huduma ya Polisi ya Malawi George Kainja, idara hiyo ilisema.

Wanne hao walitajwa na Wizara ya Mambo ya Nje kama "waliotumia vibaya nyadhifa zao za umma kwa kupokea hongo na vitu vingine vya thamani" kutoka kwa mfanyabiashara wa kibinafsi ili kubadilishana na kandarasi ya serikali.

"Marekani inasimama na Wamalawi wanaofanya kazi kuelekea taifa la haki na ustawi zaidi, kwa kukuza uwajibikaji kwa maafisa wafisadi, ikiwa ni pamoja na kutetea uwazi na uadilifu katika michakato ya ununuzi wa serikali," msemaji wawizara hiyo Matthew Miller alisema katika taarifa yake.

Forum

XS
SM
MD
LG