Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:18

Ufaransa: Moto unaotokana na ghasia waua mfanyakazi wa idara ya zimamoto


Wafanyakazi wa idara ya zimamoto wakijaribu kuzima magari yaliyowashwa moto na wanaofanya ghasia nchini Ufaransa, huko Tourcoing, Julai 2, 2023.
Wafanyakazi wa idara ya zimamoto wakijaribu kuzima magari yaliyowashwa moto na wanaofanya ghasia nchini Ufaransa, huko Tourcoing, Julai 2, 2023.

Mfanyakazi wa idara ya zimamoto  raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 alifariki Jumapili usiku  wakati akijaribu kuzima  moto kwenye magari yaliyokuwa yanaungua.

Magari hayo yalikuwa kwenye eneo la kuegesha magari chini ya ardhi kaskazini mwa Paris, wakati ghasia zikiendelea katika mji mkuu wa Ufaransa kwa usiku wa sita kutokana na polisi kumuua kijana ambaye wazazi wake ni raia wa Agleria na Morocco.

Akieleza tukio hilo, Waziri wa Usafirishaji wa Ufaransa Clement Beaune alisema: “Mawazo yangu yanakwenda kwa watumishi wa umma wakihamasisha usiku na mchana kurejea kwa utulivu.”

Mamlaka zilisema kuwa polisi wamewakamata zaidi ya watu 150 kote nchini kufuatia ghasia za usiku kucha, idadi ndogo kuliko ile ya siku zilizopita

Maafisa watatu wa polisi walijeruhiwa, ni idadi ndogo zaidi ukilinganisha na ile ya nyakati za usiku zilizotangulia.

Akizungumza katika kituo cha televisheni cha BFM Jumapili, bibi wa kijana aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi, aliwaomba wanaofanya ghasia kusitisha fujo hizo. Alitambuliwa kwa jina moja la Nadia.

Ghasia nchini Ufaransa zilipungua Jumapili usiku kufuatia maziko ya kijana huyo mapema wakati wa mchana.

Serikali imepeleka maafisa wa polisi 45,000 ili kujaribu kudhibiti ghasia hizo baada ya maziko ya Nahel, mwenye umri wa miaka 17 ambaye amezaliwa na wazazi wenye asili ya Morocco na Algeria, alipigwa risasi kwenye alama ya kusimama barabarani Jumanne katika kitongoji kilichoko nje ya Paris cha Nanterre.

Katika siku 9 za maandamano ya nyakati za usiku, wafanya ghasia wamechoma magari na kuiba madukani, wakati pia wakilenga kumbi za mijini, vituo vya polisi na shule --- majengo yanayowakilisha taifa la Ufaransa.

Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema watu 719 walikamatwa Jumamosi usiku, kidogo zaidi kuliko wale 1,311 waliokamatwa usiku uliopita na 875 waliokamatwa Alhamisi usiku.

Baadhi ya taarifa zilizomo katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG