Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 19:16

Rais Emmanuel Macron alaani kitendo cha afisa wa polisi kumua kijana wa miaka 17


Maua yawekwa kwenye eneo ambako kijana wa miaka 17 aliuawa na afisa wa polisi katika mji wa Nanterre, Juni 28, 2023
Maua yawekwa kwenye eneo ambako kijana wa miaka 17 aliuawa na afisa wa polisi katika mji wa Nanterre, Juni 28, 2023

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Jumatano amesema kifo cha kijana wa miaka 17 aliyeuawa kwa kupigwa rsiasi na afisa wa polisi siku ya Jumanne karibu na mji wa Paris, ni kitendo kisichoeleweka na kisichosamehewa, akiomba haki itendeke.

“Hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha kifo cha kijana,” amebaini rais Macron, akielezea huzuni kwa taifa zima na kudhihirisha heshima na kutoa faraja kwa familia ya kijana huyo aliyeuawa.

Nael mwenye umri wa miaka 17, aliuawa baada ya kukataa kutii amri wakati wa ukaguzi wa usafiri wa magari barabarani katika mji wa Nanterre, magharibi mwa mji mkuu Paris.

Afisa wa polisi aliyemfyatulia risasi yuko chini ya ulinzi.

“Tumeomba vyombo vya sheria kushughulikia tukio hilo mara moja, tunatumai vitafanya kazi yake kwa haraka na utulivu, na ukweli ujulikane haraka iwezekanavyo,” ameongeza rais Macron, wakati tukio hilo baya lilisababisha ghasia katika mji wa Nanterre usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG