Kupigwa risasi kwa kijana huyo kwa jina Nahel mwenye asili ya Algeria na Morocco kulipelekea maandamano makali wakati baadhi ya wakazi wakidai kuwepo kwa ubaguzi wa rangi nchini humo. Mama ya Nahel wakati akizungumza na televisheni ya France 5 alisema kwamba polisi alipoona kijana mdogo mwenye sura ya kiarabu, Alitamani kumtoa uhai.
Afisa aliyetekeleza mauaji hayo hata hivyo ameomba msamaha kwa familia. Ripoti ya polisi inasema kwamba maandamano yalipungua Jumamosi usiku wakati watu takriban 700 wakizuiliwa kulinganishwa na 1,300 waliokamatwa Ijumaa usiku.
Maafisa wamesema kwamba maafisa 45,000 wa polisi walitumwa kote nchini Ijumaa na Jumamosi ili kutuliza hali. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema kwamba maandamano hayo yanatoa fursa kwa Ufaransa, kutadhmini tatizo la ubaguzi wa rangi miongoni mwa maafisa wake.
Forum