“Rais wa Ufaransa, Macron amezungumza leo kwa njia ya simu na Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier, na kumjulisha hali ilivyo nchini mwake,” ofisi ya rais wa Ujerumani ilisema Jumamosi.
Rais Macron aliomba kuakhirishwa kwa ziara yake ya kiserikali iliyopangwa nchini Ujerumani, taarifa hiyo iliongeza kueleza.
Gazeti la Elysee lilisema mbali na hayo Macron ameelezea nia yake ya kubaki Ufaransa katika siku kadhaa zijazo kutokana na hali ilivyo nchini Ufaransa.
Hakuna tarehe mpya iliyotolewa ya ziara hiyo iliyoahirishwa chanzo kimoja cha Ufaransa kilisema. Rais wa Ujerumani, Steinmeier, amesikitika kuakhirishwa kwa ziara hiyo na kueleza kwamba anaelewa hali ilivyo katika nchi jirani, ofisi yake ilisema katika taarifa.
Alitumai kwamba vurugu za mitaani zitakwisha kwa haraka na amani kurejea.
Forum