Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:58

Ufaransa kushirikiana na Umoja wa Ulaya kuijenga tena Mayotte - Waziri


Uharibifu wa majengo uliotokana na kimbunga Chido kilichopiga eneo la Mayotte Desemba 14, 2024 katika mji mkuu Mamoudzou.
Uharibifu wa majengo uliotokana na kimbunga Chido kilichopiga eneo la Mayotte Desemba 14, 2024 katika mji mkuu Mamoudzou.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean – Noel Barrot amesema Jumatatu kwamba serikali yake itakuwa inafanya kazi na tume ya Umoja wa Ulaya kuhakikisha kwamba nguvu ya pamoja ya Ulaya iko katika nafasi ya kusaidia katika juhudi za ujenzi katika kisiwa  cha Mayotte.

Maamia au maelfu ya watu wanahofiwa kuwa wamekufa kutokana na kimbunga kibaya kilichopiga visiwa vya bahari ya Hindi karibu muongo mmoja.

Barrot alikuwa akizungumza Brussels na tayari huduma za serikali na majimbo zimeunganishwa pamoja na kutoa msaada , usalama wa raia wa Mayote ambao wanaataabika na matokeo ya janga hilo ambalo limepinga kisiwa.

Waziri wa Ufaransa kwa ajili ya maswala ya ulaya na kigeni , Jean- Noel Barrot ameeleza haya: “ Mawazo yangu yote asubuhi ya leo yako katika watu wa Mayotte ambao wanataabishwa na matokeo ya janga baya ambalo limepiga katika kisiwa.

Jean-Noel Barrot
Jean-Noel Barrot

Chini ya ya mamlaka ya Waziri Mkuu , huduma za serikali na majimbo zimeunganishwa pamoja kutoa msaada na usalama wa raia kwa ajili ya wenzetu wa mayotte.

Wiki hii tutakuwa tunafanya kazi Pamoja na tume ya umoja wa ulaya kuhakikisha kwamba umoja wetu uko sawa kusaidia juhudi za ujenzi tena zilizoko mbele yetu."

Forum

XS
SM
MD
LG