Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 10:43

Raia 22 wa Somalia wamefariki kwa ajali ya boti huko pwani ya Madagascar


Mfano wa ajali za boti barani Africa.
Mfano wa ajali za boti barani Africa.

Mamlaka ya Bandari, Bahari, na Mto Madagascar (APMF) imesema boti hizo zilisafiri kutoka Somalia kuelekea eneo la Ufaransa.

Raia wapatao 22 wa Somalia walikufa wakati boti mbili za wahamiaji zilipozama katika pwani ya Madagascar mwishoni mwa wiki, Waziri wa Habari wa Somalia Daud Aweis alisema.

Mamlaka ya Bandari, Bahari, na Mto Madagascar (APMF) imesema boti hizo zilisafiri kutoka Somalia kuelekea eneo la Ufaransa la Bahari ya Hindi la Mayotte hapo Novemba 2, safari inayochukua kilomita mia kadhaa.

Siku ya Jumamosi mamlaka ya bandari iliripoti kuwa wavuvi wa eneo hilo waligundua boti ya kwanza iliyokuwa ikielea siku ya Ijumaa karibu na Nosy Iranja. Waliwaokoa watu 25, wakiwemo wanaume 10 na wanawake 15, lakini watu saba walifariki, mamlaka hiyo imesema. Boti ya pili iliyokuwa imebeba watu 38 iliwasili katika bandari ya Madagascar, kulingana na APMF.

Mamlaka ya baharini haikuweka wazi idadi ya vifo kwa boti ya pili lakini imethibitisha kuwaokoa watu 23. Waziri wa Habari wa Somalia Aweis, akinukuu taarifa kutoka kwa wenzake nchini Madagascar, alithibitisha idadi jumla ya vifo kuwa 22.

Forum

XS
SM
MD
LG