Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:45

Upigaji kura wafanyika Comoro huku Rais Assoumani akikabiliwa na wapinzani watano


Rais wa Comoro Azali Assoumani akipiga kura katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa Urais mjini Moroni, Comoro Januari 14, 2024. REUTERS/Issihaka Mahafidhou
Rais wa Comoro Azali Assoumani akipiga kura katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa Urais mjini Moroni, Comoro Januari 14, 2024. REUTERS/Issihaka Mahafidhou

Upigaji kura ulifanyika nchini Comoro Jumapili katika uchaguzi unaotarajiwa kukabidhi muhula wa nne wa miaka mitano kwa Rais Azali Assoumani, ambaye anakabiliwa na wapinzani watano katika upigaji kura ambao baadhi ya viongozi wa upinzani wamesusia.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa kote katika visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi kuanzia saa mbili asubuhi kwa wapiga kura 338,940 waliojiandikisha kati ya watu wake 800,000. Upigaji kura ulimalizika saa kumi na mbili jioni.

Comoro imekumbwa na mapinduzi takriban 20 au majaribio ya mapinduzi tangu ili;opata uhuru wake kutoka Ufaransa mwaka 1975 na ni chanzo kikubwa cha tatizo la uhamiaji katika kisiwa kilicho karibu cha Ufaransa cha Mayotte.

\Baadhi ya viongozi wa upinzani wametoa wito wa kususia uchaguzi wakiishutumu tume ya uchaguzi kwa kukipendelea chama tawala. Tume inakanusha hili, ikisema mchakato huo utakuwa wazi.

Forum

XS
SM
MD
LG