Operesheni hiyo mpya katika kisiwa hicho cha Mayotte, imekuja mwaka mmoja baada ya kuanza operesheni ya kwanza iliyopewa jina la “Wuambushu”.
Baadhi ya maafisa wa kikosi maalumu cha polisi cha kupambana na ghasia pamoja na polisi 1,700 lazima wahusishwe katika operesheni hiyo inayojulikana kama “Mayote Place Net” ambayo ni lazima idumu kwa wiki 11.
Waziri wa Ufaransa anayeshughulika na majimbo ya n’gambo alitangaza Operesheni Act 11 itanza kwa ajili ya kurejesha utawala wa kisheria huko Mayote.
Operesheni hii mpya ya kijeshi na polisi ina lengo la kupambana na ukosefu wa usalama, uhamiaji haramu, na makazi duni ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuanza operesheni ya awali inayoitwa “Wuambushu”.
Waziri wa Ufaransa kwa ajili ya maswala ya nje Marie Guevenoux amesema “Operesheni hii ya kijeshi pamoja na polisi huko Mayote yenye lengo ya kutokomeza uhamiaji haramu na kupambana na uhalifu, itafanyika hadi mwezi Juni na kuangazia ukosefu wa usalama, uhamiaji, makazi duni na rasilimali kwa kuweka mikakati thabiti.”
“Ili kukabiliana na changamoto za usalama na kwa kushirikiana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma tunatoa kipaumbele kwa watu 60 tuliowatambua.” aliongeza.
Forum