Macron alizungumza mjini Paris mwishoni mwa mkutano wa kimataifa ulioitishwa ili kuhamasisha kuhusu umuhimu wa msaada wa kifedha, kwa juhudi ambazo ufadhili wake umepungua kwa kiasi kikubwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliitaka dunia kutosahau kuhusu watu wa Sudan, huku akitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya taifa hilo la Afrika.
"Ni vita dhidi ya maelfu ya raia ambao wameuawa, na dazani za maelfu ya watu waliojeruhiwa," aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. "Ni vita dhidi ya watu milioni 18 wanaokabiliwa na njaa kali, na jamii sasa zinatazama tishio la njaa katika miezi ijayo."
Mapigano yalizuka katika mji mkuu, Khartoum, mwaka mmoja uliopita kati ya majenerali wapinzani, mmoja akiongoza Kikosi cha Wanajeshi wa Sudan, au SAF, na mwingine Kikosi cha RSF. Uadui ulienea haraka nchi nzima.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 8 wamekimbia makwao kutafuta usalama – na milioni 1.8 kati yao wamehamia nchi jirani.
Jitihada za kuwasaidia mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa kutokana na vita zimezuiliwa na kuendelea kwa mapigano yanayoendelea, na vikwazo vilivyowekwa na pande zinazopigana, na kuathiriwa pia na ukosefu wa ufadhili wa kutosha kutoka kwa jumuiya ya kimataifa kutokana na mataifa mbalimbali pia kuhitajika kufadhili migogoro mingine ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na Gaza na Ukraine.
Forum