kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati ikishusha utabiri wake wa Pato la Taifa kwa bara hilo kutokana na kukosekana kwa utulivu wa kisiasa, ukuaji dhaifu wa kimataifa na viwango vya juu vya riba.
Katika ripoti ya Benki ya AFDB , Ukuaji halisi wa Pato la Taifa unatarajiwa kushuka kwenda asilimia 3.4 mwaka huu kutoka asilimia nne mwaka 2022, kabla ya kupanda kwendaasilimia 3.8 mwaka 2024. Mwezi Mei, ilitabiri uchumi ungepanuka kwa silimia nne kwa mwaka huu na asilimia 4.3 mwakani, baada ya kukua asilimia 3.8 mwkaa jana.
Benki hiyo aidha imetaja Athari mbaya za muda mrefu" za janga la COVID-19 pamoja na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine kupeleka bei ya chakula na nishati kupanda juu mwaka 2022 zimerudisha nyuma juhudi za kufufua uchumi wa Afrika kutoka kwa janga hilo.
Nchi nyingi za Kiafrika zimefungiwa nje ya soko la deni la kimataifa kwa viwango vya juu vya riba tangu mapema 2022, huku Ghana ikishindwa kulipa na Ethiopia ikisema inakusudia kurekebisha bondi yake moja ya nje ya nchi.
Upungufu mkubwa wa AfDB katika utabiri wa ukuaji wa 2023 ulikuwa wa Afrika ya kati, ambapo kumekuwa na mapinduzi nchini Gabon na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwenda asilimia 4.1 kutoka asilimia 4.9 mwezi Mei.
Forum