Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 15:33

Rais wa Nigeria kushiriki kikao cha G20 Ujerumani


Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu (kushoto) wakati wa Mkutano wa Viongozi wa G20 mjini New Delhi Septemba 9, 2023. Picha na Ludovic MARIN / POOL / AFP.
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu (kushoto) wakati wa Mkutano wa Viongozi wa G20 mjini New Delhi Septemba 9, 2023. Picha na Ludovic MARIN / POOL / AFP.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu atasafiri kwa ndege kwenda Berlin siku ya Jumamosi kuhudhuria kikao cha G20 Compact pamoja na kongamano la Afrika, wakati akitafuta kuvutia uwekezaji katika nishati na miundombinu pamoja na kukuza biashara, ofisi yake ilisema.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, utalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya mataifa ya Afrika na nchi za G20, msemaji Ajuri Ngelale alisema katika taarifa yake.

Rais Tinubu pia atashiriki katika mkutano wa uwekezaji wa nne wa G20, ulioandaliwa kwa pamoja na serikali ya Ujerumani, ambako atatoa hoja kwa Nigeria kama kivutio cha uwekezaji, Ngelale alisema.

Nigeria inatafuta kukuza uwekezaji badala ya kutegemea madeni ya kufufua uchumi wake ambao ukuaji wake uliodhoofishwa na rekodi ya madeni, mfumuko wa bei wa tarakimu mbili, uhaba wa fedha za kigeni na wizi wa mafuta ghafi, ambayo ni mauzo makuu ya nje.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG