Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:25

Trump asifu makubaliano yaliofikiwa na Uturuki juu ya Wakurdi


Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan

Rais wa Marekani Donald Trump alikuwa Texas Alhamisi, ambako alifanya mkutano wa kampeni katika Jiji la Dallas kutafuta kuungwa mkono katika jimbo ambalo hadi hivi karibuni lilikuwa linahisabiwa kuwa linawapigia kura Warepublikan.

Akiwa mbele ya mkusanyiko wenye shauku kubwa, Trump alijisifia juu ya Uturuki ilivyofikia makubaliano ya kusitisha mapigano baada ya Marekani kusimamia hilo, ambapo Ankara ilikubali kusitisha kwa muda operesheni ya kijeshi huko Syria ili kuruhusu vikosi vya Wakurdi kurudi nyuma katika sehemu iliyo salama.

“Turkey itakuwa na furaha, Wakurdi watakuwa na furaha, ISIS itakuwa na huzuni,” Trump alisema, akitumia jina la mkato la kikundi cha kigaidi cha Islamic State.

Makubaliano hayo yalitangazwa Alhamisi na Makamu wa Rais Mike Pence baada ya kukutana na Rais wa Uturuki Erdogan huko Ankara.

Kusitishwa kwa mapigano kumekuja wiki moja baada ya Trump kuondosha majeshi ya Marekani kutoka katika eneo linaloshikiliwa na Wakurdi huko kaskazini mwa Syria, kitu kilichompa fursa Erdogan kushambulia vikosi vya Wakurdi, YPG, na kuleta taharuki katika eneo, hali iliyosababisha wasiwasi wa kurejea tena wapiganaji wa kikundi cha Islamic State.

Kwa jumla alikosolewa kwa uamuzi huo, hata na washirika wake wa Republikan, lakini Trump alikubali kuwa utaratibu aliyotumia siyo wa kawaida.

XS
SM
MD
LG