Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:12

Trump asema Marekani itaendelea kusimama na Wakurdi


Vikosi vya Marekani kwenye mpaka wa Uturuki na Syria
Vikosi vya Marekani kwenye mpaka wa Uturuki na Syria

Rais Trump ameionya Uturuki kwamba ataichukulia hatua ambazo zitaharibu vibaya uchumi wa taifa hilo iwapo jeshi la Uturuki litashambulia wapiganaji wa Kikurdi ambao ni washirika wa Marekani katika vita dhidi ya wanaharakati wa kundi la Islamic state nchini Syria.

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza Jumanne kwamba hajawaacha pekee yao wapiganaji wa Kikurdi nchini Syria, licha ya uamuzi aliochukua wa kuondoa kikosi maalum cha Marekani nchini humo.

Rais Erdogan wa Uturuki na Rais Trump wa Marekani
Rais Erdogan wa Uturuki na Rais Trump wa Marekani

Trump aliandika kwenye ujumbe wa Twitter kwamba, hata kama wako kwenye utaratibu wa kuondoka Syria, lakini hawatowatupa kamwe wakurdi ambao ni watu wema na wapiganaji wazuri.

Lakini katika ujumbe mwengine kwenye mtandao waTwitter Rais Trump ameonekana kuipongeza Uturuki, na hata kumualika Rais Erdogan wa Uturuki kutembelea ikulu ya Marekani mwezi November, akisema Uturuki ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Marekani.

XS
SM
MD
LG