Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:08

Trump afunguliwa mashtaka ya kumuondoa madarakani mara ya pili


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumatano limepiga kura ya kumfungulia mashtaka ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump kwa mara ya pili, hatua ambayo haijawahi kutokea.

Katika kikao hicho Wademokrat waliowengi wakimtuhumu Rais Trump kwa kuchochea mapinduzi na kuhamasisha kile kilichogeuka kuwa ni shambulizi ovu katika Bunge la Marekani.

Jumla za kura zilizohesabiwa zilikuwa 232 dhidi ya 197. Warepublikan 10 waliungana na Wademokrat kupitisha uamuzi hu

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi amemuita Trump ni tishio kwa uhuru, kujitawala na utawala wa sheria.”

Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi
Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi

Lakini wafuasi wa Trump, Mwakilishi Jim Jordan wa Ohio, amesema kumfungulia mashtaka “hakuiunganishi nchi. Hii ni kuhusu siasa.” Wademokrat, amesema, “wanataka kumfuta rais huyo.”

Wingi mdogo wa Wademokrat katika Baraza la Wawakishi ulipata kura za kutosha kumfungulia mashtaka Trump wiki moja kabla ya muhula wake wa miaka minne kumalizika mchana wa Januari 20 na Mdemokrat Joe Biden ataapishwa kuwa kiongozi mpya wa nchi hii.

Idadi ndogo ya Warepublikan, hata hivyo, wameungana katika kura ambayo itampa umaarufu Trump, Mrepublikan, akiwa na hali ya kipekee katika historia ya Marekani – wa kwanza kati ya marais 45 kufunguliwa mashtaka mara mbili.

Kama Trump akishtakiwa, kesi yake itaendeshwa katika Baraza la Seneti, inatarajiwa zaidi kufanyika baada ya muda wake wa uongozi kumalizika, na itahitajika theluthi mbili ya kura katika baraza lililogawanyika kisiasa ili kumkuta na makosa.

Matokeo ya uamuzi hayana uhakika, lakini akipatikana na makosa, Baraza la Seneti katika raundi ya pili ya kura inahitaji wingi wa kura kidogo tu kumpiga marufuku kuongoza ofisi ya serikali maisha yake yote.

Baraza la Wawakilishi la Marekani
Baraza la Wawakilishi la Marekani

Baraza la Wawakilishi, bila ya kura ya Warepublikan, walimfungulia mashtaka Trump mwisho wa mwaka 2019 kwa kuitaka Ukraine kumchunguza Biden makosa yake kabla ya uchaguzi wa Novemba. Trump alikutwa bila hatia Februari baada ya siku 20 za kesi iliyoendeshwa na Baraza la Seneti.

XS
SM
MD
LG