Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 02:57

TPLF yatangaza kuwaondoa wanajeshi wake kaskazini mwa Ethiopia


Wanajeshi wa Ethiopia wakiwa ndani ya lori la kijeshi kwenye barabara inayoekea jimbo la kaskazini la Tigray.
Wanajeshi wa Ethiopia wakiwa ndani ya lori la kijeshi kwenye barabara inayoekea jimbo la kaskazini la Tigray.

Msemaji wa chama cha Tigray’s People Liberation Front ( TPLF) Jumatatu amesema wapiganaji wa chama hicho ambao wanapambana na serikali kuu ya Ethiopia, wameanza kuondoka kwenye majimbo jirani ya kaskazini mwa nchi.

Kiongozi wa TPLF, Debretsion Gebremichael ameandika kwenye barua “tunaamini kwamba kitendo chetu cha ujasiri cha kujiondoa kitakuwa ufunguzi madhubuti wa amani”.

Katika barua yake kwa Umoja wa Mataifa alitoa wito wa kutenga eneo ambako ndege hasimu haziwezi kuruka kwenye anga ya Tigray, kuiwekea Ethiopia na mshirika wake Eritrea vikwazo vya silaha, na kuunda jopo maalum la Umoja wa mataifa ambalo litahakikisha kuwa majeshi ya yameondoka huko Tigray.

Msemaji wa serikali ya Ethiopia hakujibu ombi la shirika la habari la Reuters la kutoa maelezo juu ya uamuzi huo wa TPLF.

Debretsion amesema anaamini kujiondoa kwa wanajeshi wa TPLF kutoka majimbo ya Afar na Amhara, kutailazimisha jumuia ya kimataifa kuhakikisha kwamba msaada wa chakula unaweza kuingia Tigray.

Mapendekezo mengine katika barua hiyo ni pamoja na kuachiliwa kwa wafungwa wa kisiasa. Maelfu ya Watigray wamezuiliwa na serikali. Barua hiyo inaomba pia wateuliwe wachunguzi wa kimataifa kuwafuatilia wale waliohusika na uhalifu wa kivita.

Wiki iliyopita, baraza la Umoja wa mataifa la haki za binadamu liliunda tume huru ya kuchunguza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Ethiopia, hatua ambayo ilipingwa vikali na serikali ya Ethiopia.

XS
SM
MD
LG