Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:57

Mwahabari wa kujitegemea wa AP ashikiliwa Ethiopia


Mwanahabari wa kujitegemea wa televisheni ambaye anafanyakazi na shirika la habari la Associated Press nchini Ethiopia ameshikiliwa na polisi katika mji mkuu wa Addis Ababa, shirika hilo la habari limesema Jumatano.

Amir Aman Kiyaro alishikiliwa chini ya amri ya hali ya dharura ya taifa Novemba 28 baada ya kurejea nyumbani akitokea safarini alikokuwa akiandika habari. Mpaka sasa bado hajafunguliwa mashitaka.

Maafisa wa mamlaka ya habari ya Ethiopia, ofisi ya waziri mkuu, wizara ya mambo ya nje na ofisi nyingine za serekali hazikujibu maombi kutoka shirika la habari la Associated Press kutaka taarifa za mwanahabari huyo toka alipo shikiliwa.

Chombo cha habari cha serekali Jumatano kiliripoti kushikiliwa kikitaja polisi wa serekali kuu, na kusema alikuwa akishutumiwa kwa kutumiwa na kundi la kigaidi kwa kulifanyia mahojiano.

Ripoti hiyo imesema wanahabari wa huko Thomas Engida, na Addisu Muluneh pia wanashikiliwa.

Inspekta wa polisi wa serekali kuu Tesfaye Olani aliliambia shirika la habari la serekali kwamba wanahabari hao walikiuka sheria ya hali ya tahadhari na ile ya Ethiopia ya kukabiliana na ugaidi na matendo hayo hukumu yake inaweza kuwa kuanzia miaka saba mpaka 15 gerezani.

Katika taarifa, mhariri mkuu wa shirika la habari la AP, Julie Pace ametoa mwito wa kuachiliwa kwa mwanahabari huyo na kwamba wana wasiwasi mkubwa kwamba ameshikiliwa na serekali ya Ethiopia akishutumiwa kwa ugaidi.

Ameendelea kusema kwamba mwanahabari huyo amekuwa akiandika habari za pande zote za mgogoro kwa uweledi mkubwa na wanaisihi serekali ya Ethiopia kumuachia mara moja.

XS
SM
MD
LG