Vikosi vya Tigray kutoka kaskazini mwa Ethiopia vimeukamata tena mji wa Lalibela kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na shirika la habari la Reuters.
haya yanatokea ikiwa ni chini ya wiki mbili baada ya jeshi la Ethiopia na washirika wake kuudhibiti mji huo ikiwa ni mapambano ya mpakani ambayo yalivirejesha nyuma vikosi vya Tigray mara kadhaa.
Lalibela uko katika mkoa wa Amhara ukiwa unapakana kwa kaskazini na jimbo la Tigray ambao unafahamika kwa kuwa na makanisa yaliyojengwa kwenye miamba, na umekuwa ni eneo linalo tambulika kama urithi wa dunia na Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa serekali ya Ethiopia Legesse Tulu, na msemaji wa jeshi hawakujibu kuhusiana na taarifa za kukamatwa tena kwa mji huo na vikosi vinaivyotii TPLF.
Msemaji wa TPLF Getachew Reda pia hakujibu simu za Reuters ambazo zilitaka kufahamu ukweli wa taarifa hizo.
Lakini aliweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter uliosema vikosi vyao vinafanya vizuri sana.
Mmoja wa mashuhuda ambaye alizungumza na Reuters amesema kwamba vikosi vya Amhara, ambavyo vinavyoiunga mkono serekali ya Ethiopia vilianza kuondoka Lalibela Jumamosi usiku.
Akizungumza kwa njia ya simu amesema kwamba walisikia milio ya risasi kutoka mbali usiku uliopita, lakini vikosi vya Tigray viliutwaa tena mji wa Lalibela bila ya mapambano ya risasi.
Shuhuda wa pili alilieleza Reuters, Jumapili kwamba wakazi walianza kuukimbia mji, na amesema walikuwa na hofu kwa vile hawakutegemea hilo kutokea.
Vikosi vya TPLF sasa vinafanya doria vikiwa vimevalia sare za jeshi, alisema shuhuda huyo.
Vikosi vya Tigray viliukamata mji huo mapema Agosti ikiwa ni sehemu kusonga mbele kuelekea Amhara oparesheni iliyoanza Julai.