Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:59

Masada wa chakula wa WFP waibiwa tena Ethiopia


Kwa mara ya pili katika kipindi cha siku kadhaa msaada wa chakula kwa ajili ya Waethiopia ambao wanakabiliwa na baa la njaa umeibiwa kutoka katika ghala la mpango wa chakula Duniani wa Umoja wa Mataifa (WFP) kaskazini mwa Ethiopia, Umoja wa Mataifa umesema Jumatatu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq, aliwaeleza wanahabari kwamba usiku wa Desemba 10 kundi la satu waliokuwa na silaha wanaoaminika kutoka jeshi la taifa la Ethiopia ama vikosi vyenye ushirika na jeshi, vilivamia eneo la kuhifadhi chakula la kamati ya kukabiliana na maafa ambalo lipo Kambolcha, na kuchukuwa malori 18 ya WFP kwa nguvu.

Amesema malori yaliyochukuliwa yalitumiwa na watu hao katika maeneo kadhaa kwa ajili ya shughuli zao binafsi.

Amesema malori 15 yamerejeshwa, lakini matatu mpaka sasa hayaja patikana.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa ameongeza kusema kwamba ulinzi na usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na washirika wake bado unaendelea kuwa kipaumbele cha juu, na wanataka wafanyakazi wao na washirika wake warejeshwe kwa haraka na wakiwa salama, pamoja na magari yaliyoibiwa.

WFP imeifahamisha serekali kuu ya Ethiopia, na mamlaka za kieneo katika mji wa Dessie, ambao msemaji amesema walisaidia katika kupatikana kwa malori matatu.

Miji hiyo ipo kayika mkoa wa Amhara kaskazini mwa Ethiopia ambao umeshuhudia mahitaji ya msaada yakiongezeka sana katika miezi ya karibuni.

Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 3.7 wa Amhara wanahitaji misaada ya kibinadamu kutokana na mgogoro baina ya vikosi vya serekali kjj na vile vya eneo la Tigray (TPLF).

XS
SM
MD
LG