Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 19:47

Toleo rasmi la mauaji ya waumini waliopinga kuwepo kwa UN huko DRC latiliwa shaka


Naibu Kamanda wa zamani wa Kikosi cha UN, Adrian Foster (katikati) alipolitembelea Goma Julai 29, 2012. Picha na REUTERS/James.
Naibu Kamanda wa zamani wa Kikosi cha UN, Adrian Foster (katikati) alipolitembelea Goma Julai 29, 2012. Picha na REUTERS/James.

Wiki mbili za kesi ya kijeshi kuhusu mauaji ya zaidi ya raia 50 huko mashariki mwa DR Congo, hali ya jinsi ilivyotokea na kuwafanya wanajeshi kufyatua risasi bado haijafahamika.

Nani alitoa amri hiyo, saa ngapi na kwa nini wanajeshi wa Congo walifyatua risasi kuzuia maandamano yaliyokuwa yakiupinga Umoja wa Mataifa katika mji wa Goma ni maswali muhimu lakini bado hayajajibiwa.

Mashahidi -- wengine walitoa ushahidi wakiwa wamefunika nyuso zao ili kuficha utambulisho wao -- wamelitilia shaka maelezo rasmi ya matukio.

Katika eneo ambalo limekumbwa na ghasia kwa muda mrefu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tukio hilo limeibua hali ya wasiwasi.

Tarehe 30 Agosti, wanajeshi waliyazuia madhehebu ya kidini kufanya maandamano yaliyokuwa yakipinga uwepo wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC.

Takriban watu 57 waliuawa, kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani Peter Kazadi.

Chini ya wiki moja baada ya msako kufanyika, wanajeshi sita wakiwemo maafisa wawili wa kikosi cha elite Republican Guard walifikishwa mahakamani wakishtakiwa kwa tuhuma za kukiuka amri na uhalifu dhidi ya ubinadam.

Takriban watu watano waliuawa katika majengo ya redio ya dhehebu hilo la kidini, lakini wengi wao walifia kanisani, kulingana na ushahidi uliotolewa.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP


Forum

XS
SM
MD
LG