Watoto hao wa kike waligundulika katika kijiji kimoja kilichopo Kivu Kaskazini, eneo ambalo kundi la wanamgambo linalojulikana kama Allied Democratic Forces (ADF) limezidisha mashambulizi ya mabomu, shirika linaloshughulikia watoto la UNICEF limesema.
Vilipuzi hivyo vilifanikiwa kuondolewa na wataalamu wa kutegua milipuko.
"Azma ilikuwa kuwalenga polisi au wanajeshi wa Congo walipowasili na kuchochea mlipuko dhidi ya majeshi ya usalama" mwakilishi wa UNICEF nchini Congo, Grant Leaity, aliuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Geneva.
Mapacha ambao hawajatambuliwa, sasa wanapatiwa huduma
kutokana na utapiamlo katika kituo cha Umoja wa Mataifa kabla ya kupelekwa katika kituo cha malezi.
Wazazi wao wameuawa katika shambulio linaloaminika kutekelezwa na ADF. Ingawa watoto hao wanaendelea vizuri,
makovu ya kiakili yanaweza kudumu maisha yao yote, Leaity alisema.
Wakatai huo huo, wanaume wenye silaha wamekishambulia kijiji kimoja katika jimbo la Ituri mashariki mwa Congo siku ya Alhamisi, na kuua takriban watu 18 na kujeruhi 12, afisa wa eneo hilo alisema.
Kanali Jean Siro Simba Bunga, msimamizi wa eneo la Irumu ambako shambulio hilo lilitokea, alisema washambuliaji walichoma miili mitatu lakini mingine 15 itazikwa.
Eneo hilo lililogubikwa na idadi kubwa ya makundi yenye silaha na vurugu imewalazimu mamilioni kuyakimbia makazi yao.
Chanzo cha taarifa hii ni shirika la habari la Reuters
Forum