Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:45

Wanamgambo wasiojulikana wavamia eneo la mgodi DRC na kuua watu 13


Mchimba madini katika eneo la wachimbaji wadogowadogo huko Kalimbi kaskazini mwa Bukavu, Machi 30, 2017. Picha na GRIFF TAPPER / AFP.
Mchimba madini katika eneo la wachimbaji wadogowadogo huko Kalimbi kaskazini mwa Bukavu, Machi 30, 2017. Picha na GRIFF TAPPER / AFP.

Wanamgambo wasiojulikana wamewauwa takriban watu 13 usiku wa kuamkia Jumanne, kwenye machimbo ya dhahabu huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, msemaji wa jeshi na kiongozi wa mashirika ya kiraia alisema.

Shambulio hilo lilitokea Jumatatu jioni katika eneo lenye machimbo ya madini ya shaba linalomilikiwa na watu binafsi huko Aru, karibu na mpaka kati ya Uganda na jimbo la Ituri, alisema Dieudonne Lossa, rais wa jumuiya kiataifa wa jimbo la Ituri.

Watu kumi na watatu wameuawa, tisa wamejeruhiwa vibaya na wengine kadhaa kuchukuliwa mateka na washambuliaji ili kusafirisha dhahabu na bidhaa zao nyingine walizoziiba, Lossa aliliambia shirika la habari la Reuters.

Alisema kuwa makundi mawili yenye silaha yanafanya harakati zao katika eneo hilo: Ushirika wa Maendeleo ya Congo (CODECO), na wanamgambo hasimu wanaoitwa Zaire, ni miongoni mwa dazeni ya wanamgambo wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mashariki lililogubikwa na migogoro.

Hapo awali Lossa aliilaumu CODECO, ambayo inadai kutetea maslahi ya wakulima wa kabila la Lendu dhidi ya wafugaji wa kabila la Hema, kwa mashambulio tofauti yaliyoua takriban watu 14 katika kanisa moja lililoko katika jimbo la Ituri siku ya Jumapili.

Hakuna madai yaliyotolewa mara moja ya kuhusika na shambulio hilo, na wawakilishi wa CODECO na Zaire hawakuweza kupatikana kutoa maoni kuhusiana na shambulio hilo.

Msemaji wa jeshi la Ituri, Jules Ngongo Tshikudi ametaja idadi ya vifo kutokana na shambulizi hilo katika machimbo wamefikia 14 na hakusema nani anahusika.

"Operesheni zinaendelea katika eneo hili ili kukomesha matukio ya watu hawa wenye silaha ambayo yameota mizizi na kuwa tishio katika ukanda huu ulioko kwenye mpaka na Uganda," alisema Tshikudi.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG