Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:33

Viongozi wawili wa waasi wauawa na jeshi la Msumbiji

Ramani ya Msumbiji
Ramani ya Msumbiji

Jeshi la Msumbiji limewaua viongozi wawili wakuu wa waasi akiwemo naibu wa kamanda, jeshi la ulinzi la nchi hiyo lilitangaza Jumatano.

"Gaidi Abu Kital, ambaye alishika nafasi ya naibu kamanda wa operesheni za kundi la kigaidi la Al Sunna Wall Jammat, alipigwa risasi" vikosi vya ulinzi vya Msumbiji (FADM) vilisema katika taarifa.

Ali Mahando ambaye "alishikilia nyadhifa muhimu ndani ya kundi la kigaidi" pia aliuawa, taarifa hiyo iliongeza.

Jimbo la kaskazini mwa Msumbiji lenye utajiri wa gesi, Cabo Delgado, linapambana na uasi unaoendeshwa na wanamgambo wanaohusishwa na kundi la Islamic State.

Kwa mujibu wa FADM, jeshi la ulinzi na mamlaka za usalama zilivamiwa na wanachama wa kundi hilo la waasi katika wilaya ya jimbo lenye machafuko, wakati gari lao "lilipopinduka kwenye daraja, na kisha kuwaka moto".

Vikosi vya usalama "vilitoroka bila kujeruhiwa" na viongozi wa waasi waliuawa katika mapigano yaliyofuata, vikosi vya jeshi vilisema.

Taarifa ya jeshi hilo haikueleza ni lini tukio hilo lilifanyika, lakini ripoti nyingine zilidokeza kuwa lilitokea Jumanne.

Uasi huo ulianza Oktoba 2017 wakati wapiganaji – ambao baadaye walijitambulisha kama kuwafuasi wa kundi la Islamic State -- walishambulia maeneo ya pwani kaskazini mwa Cabo Delgado, karibu na mpaka wa Tanzania.

Forum

XS
SM
MD
LG