Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:23

Kenya, Ghana na Malawi kupokea chanjo dhidi ya Malaria


Mtoto akipewa chanjo dhidi ya Malaria katika hospitali ya Lumumba, Kisumu, Kenya. July 1, 2022
Mtoto akipewa chanjo dhidi ya Malaria katika hospitali ya Lumumba, Kisumu, Kenya. July 1, 2022

Shirika la afya duniani WHO, na washirika wake wamesema kwamba karibu dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria duniani, zitatolewa kwa nchi 12 za Afrika ifikapo mwaka 2025.

Kati ya nchi zintakazopokea chanjo hiyo ni Malawi, Ghana na Kenya, ambapo chanjo dhidi ya Malaria, ya Mosquirix imeshatumika wakati wa majaribio.

Kutokana na kuwepo mahitaji mengi ya chanjo hiyo, nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi ya Malaria ndio zitakazozingatiwa zaidi.

Msumbiji na Sudan zimeondolewa kwenye orodha hiyo kutokana na viwango vya juu vya kutotumia chaanjo inapozinduliwa.

Shirika la afya duniani limesema kwamba chanjo hiyo imetengenezwa na kmpuni ya Uingereza yaa GSK, na kwamba chanjo hiyo itaokoa Maisha ya angalau mtoto mmoja kati ya 200 watakaopokea chanjo.

Malaria huua karibu watoto nusu milioni walio na umri wa chini ya miaka mitano barani Afrika kila mwaka.

Forum

XS
SM
MD
LG