Mkuu wa zamani wa idara ya wanyamapori ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na wafanyakazi wenzake wawili wa zamani wamewekwa katika orodha ya vikwazo vya Marekani kutokana na kusafirisha kinyume cha sheria sokwe, jamii ya sokwe na viumbe wengine waliohifadhiwa Marekani imesema.
Watatu hao wamezuiliwa kuingia Marekani kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani iliyotolewa Jumatano. Hatua hiyo imewekwa kwa Cosma Wilungula, mkurugenzi mkuu wa zamani wa Taasisi ya Hifadhi ya Mazingira ya Congo (ICCN), Leonard Muamba Kanda, mkuu wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyekuwa anasimamia utekelezaji wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa wa Viumbe Walio hatarini (CITES) na mkurugenzi wa ICCN, na Augustin Ngumbi Amuri, mratibu wa CITES na mshauri wa kisheria wa ICCN.
Kama maafisa wa umma wanaohusika na ulinzi wa wanyamapori walitumia vibaya nafasi zao za umma kwa kusafirisha kinyume cha sheria sokwe na wanyamapori wengine waliohifadhiwa kutoka DRC kwenda Jamhuri ya Watu wa China kwa kutumia vibali vya uongo, kwa kupewa hongo, ilisema taarifa hiyo.
Forum