Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:56

Mwandishi wa habari mashuhuri nchini DRC apelekwa jela kwa tuhuma za kusambaza habari za uongo


Rais wa DRC Felix Tshisekedi akihudhuria hafla ya kuapishwa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mjini Harare, Septemba 4, 2023
Rais wa DRC Felix Tshisekedi akihudhuria hafla ya kuapishwa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa mjini Harare, Septemba 4, 2023

Mwandishi wa habari mashuhuri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amepelekwa jela baada ya kukamatwa kwake, mwajiri wake amesema, licha ya makundi ya kutetea haki na balozi za kigeni nchini humo kuomba aachiliwe huru.

Maafisa wa DRC wiki iliyopita walimuweka kizuizini mwanahabari Stanis Bujakera ambaye anafanya kazi na shirika la habari la Reuters na jarida la Jeune Afrique, kwa tuhuma za kusambaza habari za uongo.

Kukamatwa kwake kulifuatia habari iliyochapishwa na Jeune Afrique mwishoni mwa mwezi Agosti, ikidai kwamba idara ya kijasusi ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiyo ilimua mwanasiasa wa upinzani Cherubin Okende mwezi Julai.

Makala hiyo ambayo haikuwa na jina la mwandishi huyo wa habari, ilinukuu waraka wa siri kutoka idara tofauti ya kijasusi.

Maafisa wa DRC walisema waraka huo ni ghushi.

Bujakera, ambaye anafanya kazi pia na gazeti la mtandaoni la DRC, Actualite cd alikamatwa tarehe 8 Septemba na kuwekwa kizuizini kabla ya kufikishwa kwa mwendesha mashtaka.

Mkurugenzi wa gazeti la Actualite cd aliiambia AFP jana Alhamisi kwamba Bujakera alihamishwa kwenye jela maarufu ya Makala katika mji mkuu Kinshasa.

Forum

XS
SM
MD
LG