Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:27

Tinubu awaachisha kazi maafisa wa jeshi, polisi


Raia wa Nigeria, Bola Tinubu
Raia wa Nigeria, Bola Tinubu

 Rais wa Nigeria Bola Tinubu alifanya mabadiliko makubwa kwa vikosi vya ulinzi Jumatatu, na kuwasimamisha kazi wakuu wa usalama na mkuu wa polisi chini ya mwezi mmoja baada ya kuingia madarakani.

Tinubu, ambaye aliapishwa tarehe 29 mwezi Mei, amifanya sekta ya usalama moja ya vipaumbele vyake vikuu na kuahidi mageuzi, ikiwa ni pamoja na kuajiri askari zaidi na maafisa wa polisi, huku akiwaongezea mishahara bora na kuwapatia vifaa bora zaidi.

Wanajeshi wa Nigeria wamekuwa wakipambana na waasi wa kiislamu kwa muda mrefu katika maeneo ya kaskazini masharik mwa nchi, huku visa vya ujambazi na utekaji nyara kwa lengo la kulipwa fidia, vikiongezeka katika eneo la kaskazini magharibi, wakati ukosefu wa usalama ukienea katika maeneo mengi ya nchi.

Siyo kawaida kwa rais mpya wa Nigeria kuwalazimisha wakuu wa usalama kustaafu mapema baada ya kuchukua madaraka, kama Tinubu alivyofanya Jumatatu.

Alimchagua Nuhu Ribadu, afisa mkuu wa zamani wa polisi na mkuu wa zamani wa mamlaka ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi na kifedha nchini, kama Mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa.

Meja Jenerali Christopher Musa, ambaye hadi mwaka jana alikuwa akiongoza mapambano ya jeshi dhidi ya waasi, anachukua nafasi ya mkuu mpya wa majeshi kutoka kwa Lucky Irabor. Tinubu pia aliwateua makamanda wapya wa jeshi la ardhini, la wanamaji na la anga pamoja na mkuu mpya wa Huduma ya Forodha ya Nigeria.

Forum

XS
SM
MD
LG