Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:32

Tinubu atetea uamuzi wa serikali yake kuondoa ruzuku ya mafuta ya magari


Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu

Rais wa Nigeria Bola Tinubu siku ya  Jumatano alitetea uamuzi wa wiki iliyopita wa taifa hilo la Afrika Magharibi kuacha kutoa ruzuku ya mafuta.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari hatua hiyo imeongeza bei ya usafirishaji na bidhaa nchini humo.

Tinubu aliomba kuwepo uvumilivu katika kipindi ambacho mamilioni ya wananchi nchini Nigeria wanakabiliwa na matatizo ya ziada ya kiuchumi.

Pesa zilizookolewa kwa kuondoa ruzuku ya miongo kadhaa zitasaidia juhudi za serikali za kupambana na umaskini,

Pia fedha hizo zitatumika kutekeleza mipango mingine, Tinubu aliwaambia magavana walihodhuria mkutano katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja.

Taarifa kutoka ikulu ya rais wa Nigeria ilimnukuu Tinubu akisema "tunaweza kuona athari za umaskini kwenye nyuso za watu wetu. Umaskini si wa kurithi, ni wa jamii. Msimamo wetu ni kuondoa umaskini."

Magavana waliunga mkono kuondolewa kwa ruzuku hiyo na kuahidi kufanya kazi pamoja katika kutekeleza, taarifa ya rais ilisema.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG