Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 18:41

Rais wa Nigeria asaini mswaada wa aina yake wa mkopo kwa wanafunzi


Rais wa Nigeria Shugaba Bola Tinubu
Rais wa Nigeria Shugaba Bola Tinubu

Rais mpya wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu amesaini mswaada kuwa sheria ya mkopo wa wanafunzi ambao unasemekana ni wa kipekee na aina yake nchini humo.

Sheria hiyo inatarajiwa kuwasaidia wanafunzi maskini katika kujipatia elimu ya juu.

Wanafunzi ndani ya nchi hiyo ambao sasa wanahudhuria vyuo vikuu, vyuo vya kawaida na kiufundi wataweza kukopa kiurahisi bila kulipa riba kutoka bodi ya mkopo ya Wizara ya Elimu ya Nigeria kwa ajili ya kulipia ada zao.

Mwezi Novemba, Bunge la Nigeria lilipitisha mswaada wa kuitaka benki ya elimu kutoa mikopo kwa wanafunzi.

Lakini rais wa zamani Muhammadu Buhari alishindwa kusimamia mswaada huo hadi alipoondoka madarakani Mei 29, hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa kuhusu kwa nini hatua hazikuchukuliwa.

Mswaada huo uliwasilishwa na mkuu wa utawala wa Bwana Tinubu mwaka 2016 Femi Gbajabiamila wakati alipokuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi.

Forum

XS
SM
MD
LG