Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:31

Tetemeko la ardhi latikisa California wakati dhoruba 'Hilary' ikisababisha mafuriko makubwa


Magari ya kuzima moto yanaonekana katika eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi Kaskazini mwa mji wa Los Angeles.
Magari ya kuzima moto yanaonekana katika eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi Kaskazini mwa mji wa Los Angeles.

Wakati eneo la Kusini mwa jimbo la California likikumbwa na dhoruba isiyo ya kawaida ya msimu wa  kiangazi Jumapili alasiri, tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.1, cha rikta, pia liligonga eneo hilo, kwa mujibu wa idara ya Jiolojia ya Marekani.

Shirika la habari la CNN liliripoti Jumapili jioni kwamba Kitovu cha tetemeko hilo kilikuwa ni eneo la Ojai, kati ya miji ya Santa Barbara na Ventura, likiinukuu idara hiyo.

Hakukuwa na ripoti za mara moja za uharibifu, Sheriff wa Kaunti ya Ventura alisema katika ujumbe uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Awali, mafuriko makubwa yalikumba mitaa kadhaa katika eneo kame la Mexico la Baja California, siku ya Jumapili wakati Dhoruba Hilary iliposonga ufukweni ikisababisha mvua kubwa, ikielekea Kusini mwa California, na kusababisha wasiwasi kuongezeka kwamba mafuriko makubwa huenda yakatokea katika maeneo ya kaskazini kama jimbo la Idaho ambako ni nadra kupata mvua kubwa kama hiyo.

Watabiri walisema Hilary ilikuwa dhoruba ya kwanza ya kitropiki kupiga eneo la kusini mwa California katika miaka 84, na kuleta uwezekano wa mafuriko makubwa, maporomoko ya ardhi, vimbunga, upepo mkali na kukatika kwa umeme.

Hilary ilitua kwenye pwani ya Mexico katika eneo lenye idadi ndogo ya wakazi, takriban kilomita 150 kilomita 250 kusini mwa Ensenada, ikielekea eneo la Tijuana Jumapili jioni, na kutishia makazi ya muda kwenye milima iliyo kwenye mpaka wa Kusinni mwa Marekani.

Takriban watu milioni 9 walitahadharishwa juu ya mafuriko hayo, wakati mvua kubwa ikinyesha kusini mwa California kabla ya dhoruba hiyo. Watabiri walionya kwamba maeneo ya jangwani huenda yakaathiriwa zaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG