Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 16:47

Utawala wa Biden unakubali kurekebisha mkakati wake wa COVID-19


Mfano mmojawapo wa chanjo za COVID-19
Mfano mmojawapo wa chanjo za COVID-19

Wakati upatikanaji wa chanjo ulimwenguni ukizidi uwezo wa usambazaji utawala wa Biden unakubali kuna umuhimu wa kurekebisha mkakati wake wa kukabiliana na janga la COVID-19 ili kushughulikia vikwazo vinavyokabili nchi za kipato cha chini kupata chanjo kwa raia wao.

Ni wazi kwamba ugavi unazidi mahitaji na eneo linalolengwa linahitaji sana kupata chanjo hiyo inayochomwa mkononi, alisema Hilary Marston, mshauri mwandamizi wa sera za COVID kwa ulimwengu aliiambia VOA.

Hilo ni jambo ambalo tunalizingatia kwa mwaka 2022. Marston alisema kwamba utawala umesaidia kuongeza usambazaji wa chanjo duniani kupitia michango, kupanua uwezo wa utengenezaji wa chanjo ulimwenguni, na msaada kwa COVAX, utaratibu wa kimataifa wa kushiriki chanjo unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na taasisi za afya za GAVI na CEPI.

Kufuatia shida ya usambazaji wa chanjo hapo mwaka 2021 usambazaji wa COVAX sio kikwazo tena, msemaji wa GAVI aliiambia VOA. Alisema COVAX hivi sasa ina uwezo wa kuzingatia kuunga mkono mikakati ya nchi, uwezo, na mahitaji.

XS
SM
MD
LG