Hii itakuwa ni mara yake ya tatu kuwania, baada kumshinda mgombea wa Demokrat, Hilary Clinton mwaka 2016, na aliposhindwa kutetea kiti chake katika uchaguzi wa 2020.
Akiwa katika makazi yake ya Mar-a-Largo, Trump ametoa tangazo hilo huku wachambuzi wakiona ni kama kupuuzia madai ya Waripablikan kwamba ni yeye aliyechangia kukosekana kwa wapiga kura wengi.
Mpaka sasa bado analalamika kwamba uchaguzi uliopita alifanyiwa hila zilizo muwezesha rais wa sasa wa 46, Joe Biden kushinda.
Hata hivyo anakabiliwa na hali ngumu ya kisiasa licha ya kwamba kasi yake inaonekana kutozingatia hilo.
Trump ametoa tangazo hilo akiwa na wasaidizi wake kisiasa pamoja na wafuasi wake katika makazi yake ya Mar-a-Largo yaliyopo katika jimbo la kusini la Florida, ambayo amekuwa akiishi toka alipo ondoka madarakani mjini Washington, Januari mwaka jana.