Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 21:00

Kimbunga Hilary kutua California mwishoni mwa wiki kikitokea Mexico


Picha ya satellite ikionyesha kimbunga Hilary kikiwa kwenye bahari ya Pacific karibu na Mexico/ Agosti 17, 2023.
Picha ya satellite ikionyesha kimbunga Hilary kikiwa kwenye bahari ya Pacific karibu na Mexico/ Agosti 17, 2023.

Kituo cha kitaifa cha vimbunga hapa Marekani kimesema Alhamisi kwamba kimbunga Hilary kimeongezeka kasi na kufikia kiwango cha pili karibu na ufukwe kwa Mexico wa Pacific, kikitarajiwa kusababisha mvua kubwa kusini magharibi mwa Marekani kufikia mwishoni mwa wiki.

Taarifa zimesema kwamba kimbunga Hilary kina upepo wa kasi ya kilomita 165 kwa saa na huenda kikapiga katika ufukwe wa Baja kwenye penisula ya California kufikia mwishoni mwa wiki.

Hilary kilionekana takriban kilomita 805 kusini- kusini mashariki mwa Los Cabos kwenye ukingo wa kusini mwa peninsula ya Baja. Ingawa kilikuwa mbali na nchi kavu, kililikuwa kilielekea magharibi – kaskazini magharibi kwa kasi ya kilomita 22 kwa saa, kilitarajiwa kugeukia upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Marekani.

Kulingana na idara ya kitaifa ya hali ya hewa ya Marekani, hakuna kimbunga kingine kilichopiga kusini mwa California tangu Septemba 25, 1939.

Forum

XS
SM
MD
LG