Eneo hilo linalotambuliwa na Unesco kama hifadhi ya kimataifa nchini humo litaiwezesha Tanzania kuwa na uwezo wa uzalishaji umeme zaidi ya mara mbili.
Hifadhi hiyo ya wanyama ya Selous ni eneo lililotengwa upande wa kusini mwa Tanzania. Lina jumla ya Kilomita za mraba 50,000 na maeneo mengine yanayolindwa.
Eneo hilo lilitengwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa, UNESCO, kuwa ni eneo la hifadhi ya kimataifa mwaka 1982 kutokana na kuwepo wanyama pori wa aina mbalimbali na hali ya tabia nchi kuwa ni asilia.
Mradi huo umepata upinzani kutoka kwa wanaharakati wa mazingira na hifadhi ambao wamesema ujenzi wa bwawa kupitia hifadhi ya Selous nchini humo utaharibu mazingira na maumbile ya tabia nchi ikiwemo malisho na makazi ya wanyama pori.
Upinzani huo unatokana na eneo hilo kuwa ni hifadhi maarufu ya wanyama pori kama Tembo, vifaru weusi na Twiga na wanyama wengine kadhaa kunaweza kuathiri maisha ya wanyama pori na makazi yao.
Waziri wa nishati wa Tanzania Medard Kalemani, amesema mradi huo utakuwa na ukubwa wa megawati 2115 na kusema ni mradi mkubwa sana.