Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:59

Tanzania kuendelea na mradi wa umeme Selous


Eneo la Stiegler’s Gorge Tanzania
Eneo la Stiegler’s Gorge Tanzania

Tanzania imelifahamisha shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuwa mradi wa umeme unaoendelea eneo la Stiegler’s Gorge hauwezi kusitishwa.

Wizara imesema katika tamko lake lililotolewa Dar es Salaam Jumatatu kwamba Meja Jenerali Milanzi alidai mbele ya Kamati ya Urithi wa Dunia (WHC) kwamba mpango wa kujenga mradi wa kuzalisha umeme ulikuwa tayari katika ajenda ya serikali ya Tanzania tangia mwaka 1960.

Mradi huo unaotekelezwa katika hifadhi ya wanyama pori huko Selous umezua mjadala mkali ambapo wanaharakati wa mazingira wanapinga mradi huo kutekelezwa kwa sababu utaangamiza urithi wa dunia.

Lakini wakati wa mkutano wa WHC ya UNESCO huko Poland wiki iliopita, ujumbe wa serikali ulitoa msimamo thabiti wa kuendelea na utekelezaji wa mradi huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mali Asili na Utalii, Meja Generali Gaudence Milanzi aliongoza timu ya Tanzania ambayo pia alikuwepo katika ujumbe huo Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Samwel Shelukindo ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa UNESCO.

Hifadhi hiyo ya wanyama pori ya Selous yenye eneo la kilomita za mrada 50,000 na pendekezo hilo la mradi huo unategemea kutumia asilimia 3 ya eneo hilo. Katibu Mkuu aliendelea kushikilia kwamba hifadhi hiyo ya wanayama pori ya Selous ilikuwa tayari imeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.

“Ni lazima izingatiwe kuwa wakati eneo hilo linafanywa kuwa hifadhi mwaka 1982, Shirika la kimatiafa la hifadhi ya mazingira (IUCN) ilikuwa haijaona kuwa mradi wa Stieglers Gorge (mradi wa kuzalisha umeme) ni tishio kubwa la mazingira hasa ukizingatia ukubwa wa eneo hilo.

XS
SM
MD
LG