Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:02

Tanzania: Serikali yapandisha kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wake


Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia taifa baada ya kula kiapo
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia taifa baada ya kula kiapo

Serikali ya Tanzania imetangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa umma nchini humo kwa 23.3%.

Rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Samia Suluhu Hassan amesema ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara yaliyo wasilishwa Ikulu, ikiwa ni muendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alipokea taarifa ya watalaamu mjini Dodoma kuhusu suala la nyongeza ya mshahara.

“Nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi', ilisema taarifa ya Ikulu.

Kulingana na taarifa hiyo serikali inatarajiwa kutumia shilingi trilioni 9.7 kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote wa serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na idara nyingine za Serikali.

Kutokana na nyongeza hiyo ya mishahara, bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/2023 itaongezeka kwa shilingi trilioni 1.59 sawa na asilimia 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya sasa ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Wakati huo huo Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya mafao ya pensheni, kama ilivyoombwa na chama cha wafanyakazi Tanzania (TUCTA) siku ya sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi, 2022).

Rais aimekubali ombi la kupandisha malipo ya mafao, kutoka 25% ambayo ilikataliwa hapo awali na wadau hadi 33.3%.

Pia amewataka TUCTA, wizara ya fedha na Chama cha Waajiri (ATE), kuendelea kushirikiana ili kukamilisha taratibu za malipo ya mkupuo huo wa asilimia 33.3% badala ya 25% iliyokataliwa mwaka 2018.


XS
SM
MD
LG