Kabla ya mkutano huo, Harris aliwaeleza wana habari kuwa maeneo matatu ya majadiliano ni kuimarisha demokrasia, uwekezaji and ukuaji uchumi, na afya ya ulimwengu.
“Utawala wetu una nia ya dhati kuimarisha mahusiano na Tanzania na nchi za Afrika kwa jumla,” Harrisi alisema. “Hili limekuwa eneo ambalo tumelitupia jicho na kuweka kipaumbele kwa wote, Rais Joe Biden na mimi.”
Rais Samia, alipanda cheo baada ya kuwa makamu rais wakati wa utawala wa John Magufuli ambaye alifariki March mwaka 2021, na kuashiria kuwa anataka kusukuma mbele sera za mambo za Tanzania na kuvutia uwekezaji zaidi wa kigeni. Kwa hilo, alikutana na viongozi wa Beijing, London, Brussels, Moscow na Ghuba.
Alitumia hotuba yake kwenye kikao cha 76 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) mwezi Septemba – kwa mara ya kwanza kiongozi wa Tanzania alihutubia baraza hilo tangu mwaka 2015 – kuiuza nchi yake kama mshirika wa biashara, kuahidi mabadiliko ya sera rafiki za kibiashara.
Serikali yangu ingependa kuona uhusiano wetu unakua zaidi na kuimarishwa kwa viwango vya juu,” Samia alimueleza Harris. “Ombi langu hapa ni kuiomba serikali ya Marekani kushawishi uwekezaji zaidi kutoka sekta binafsi kutoka Marekani kuja kufanya kazi na sisi.”
“Tunapongeza maendeleo mliyoyafikia wakati wa uongozi wako na hususan jitihada zako za kuwawezesha viongoiz wanawake nchini Tanzania na kazi ya kuunga mkono haki za binadamu,” amesema Kamala.
Tanzania ni moja ya nchi 11 za Afrika ambazo zinanufaika na msaada wa Marekani kupitia mpango wa ulimwengu wa fursa ya chanjo maarufu kama Global VAX ili kuboresha viwango vya utoaji wa chanjo ya Covid-19 katika katika mataifa yanayoendelea.