Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:28

Suala la uraia pacha halipo kwa sasa -Samia Suluhu


 Watanzania wanaoishi Marekani wakiwa nje ya Ubalozi wao uliopo Washington DC wakiwa na mabango wakimsubiri rais Samia Suluhu Hassan.
Watanzania wanaoishi Marekani wakiwa nje ya Ubalozi wao uliopo Washington DC wakiwa na mabango wakimsubiri rais Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesisitiza nia ya serikali yake kutoa hadhi maalum kwa watanzania wanaoishi ughaibuni badala ya uraia pacha.

Akizungumza na wanadiaspora katika hoteli ya Marriott mjini Washington DC Jumamosi Rais Samia ameelezea miradi na kazi anazofanya katika awamu yake ya uongozi akisema wakiendeleza ujenzi wa vituo vya afya ikiwa ni miradi zaidi ya 500, miundo mbinu na pamoja kupambana na Malaria.

Amesema hadhi maalum watakayopewa watanzania wanaoishi nje ya nchi itawapa fursa ya kumiliki ardhi,urithi na mengineyo na wanashughulikia sera ya diaspora na wizara ya mambo ya nje wataisambaza kwa wadau wa diaspora ili nao wachangie mawazo yao kabla ya kuirasimisha. Akisisitiza suala la uraia pacha halipo kwa sasa.

Wakati huo huo nje ya hoteli hiyo alipokelewa na watanzania waliokuwa na ujumbe kwa rais huyo wakidai kuna haja kwa taifa kuwa na katiba mpya , uhuru wa habari na kutendewa haki kwa wanasiasa wa upinzani pamoja na kutaka kujua wale waliopotea wako wapi.

Rais alitambua kupokea ujumbe wa watanzania hao “aliowaita ni watoto wake pia” akisema ameanzisha mazungumzo ya maridhiano na vyama vya siasa kupitia baraza lao wakiwemo polisi,viongozi wa dini na taasisi za kijamii ili kujadili mipango yao na kumpelekea ripoti ili waamue lipi waanze nalo akizungumzai chama kimoja cha siasa bila ya kukitaja jina kwamba bado hakijajiunga lakini anaendelea na mazungumzo nao.

Amesema amefanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Marekani na kusaini MOU zenye thamani ya zaidi ya shilingi za kitanzania trilioni moja ikiwa ni ushirkiano wa kibiashara na siyo kuomba misaada yaani sekta binafsi ya Marekani na Tanzania iwekeze na kwa pamoja halafu wagawane faida.

Rais huyo amekutana na makamu rais wa Marekani Kamala Harris, wafanyabiashara , taasisi za kidemokrasia na IMF na wakati huo huo akizindua filamu ya Royal Tour ya kutangaza utalii wa Tanzania katika miji mikubwa ya biashara ya Marekani New York na Los Angeles na kukutana na jumuiya za watanzania.

Huku akisisitiza kuboresha mahusiano ya Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa.

XS
SM
MD
LG