Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 18:39

Somalia yamuondoa balozi wa Ethiopia aliyeko Mogadishu


Wanawake wakiwa wameshika bendera ya Somalia wakiimba wakati wa maandamano kuiunga mkono serikali ya SomaliaJanuari 3, 2024. Picha na ABDISHUKRI HAYBE / AFP
Wanawake wakiwa wameshika bendera ya Somalia wakiimba wakati wa maandamano kuiunga mkono serikali ya SomaliaJanuari 3, 2024. Picha na ABDISHUKRI HAYBE / AFP

Somalia imemrudisha nyumbani balozi wa Ethiopia aliyekuwa Mogadishu kwa mashauriano siku ya Alhamisi na kufunga ofisi mbili za ubalozi mdogo katika eneo la Puntland lisilo na mamlaka kamili na lililojitenga kutoka Somalia.

Hatua hiyo inafuatia mzozo unaohusiana na mpango wa Ethiopia wa kukodisha eneo la pwani nchini Somalia.

Msemaji wa waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Nebiyu Tedla amesema , Ethiopia haikuwa na taarifa kuhusiana na suala hilo ambalo limetangazwa na ofisi wa waziri mkuu wa Somalia.

“Uingiliaji wa wazi wa serikali ya Ethiopa katika masuala ya ndani ya Somalia ni ukiukwaji wa uhuru na mamlaka ya Somalia” ofisi ya waziri mkuu wa Somalia imesema katika taarifa.

Maafisa wawili wa Somalia wamesema hatua hiyo inahusiana na mzozo kuhusiana na hati ya maelewano Ethiopia iliyoikubali Januari mosi, kukodi kilometa 20 za eneo la pwani huko Somaliland- sehemu ya Somalia ambayo inadai ina uhuru na imekuwa na mamlaka tangu mwaka 1991.

Ethiopia imesema inataka kuweka kambi ya jeshi la majini katika eneo hilo na kupendekeza uwezakano wa kutambuliwa kwa Somaliland – na kuzua majibu makali kutoka Somalia na hofu ya mpango huo kuliyumbisha zaidi eneo hilo la Pembe ya Afrika.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, awali aliuita mpango huo wa bandari ni kinyume cha sheria na alisema Februari nchi yake "itajilinda" endapo Ethiopia itaendelea na mpango huo.

Hatua ya kumuondoa balozi na kuzifunga ofisindogo za kibalozi imezua wasiwasi kuhusiana na hatma ya wanajeshi wa Ethiopia 3,000 walioko Somalia kama sehemu ya misheni ya Umoja wa Afrika ya kulinda Amani inayopambana na al Shabaab, washirika wa al Qaeda.

Forum

XS
SM
MD
LG