Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 07:51

Sikukuu ya 'Thanksgiving' yawakutanisha wakimbizi walioko eneo la Washington


Wakimbizi wafarijika kwa kuwezeshwa kukutana na kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving Marekani
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:46 0:00

Wakimbizi wafarijika kwa kuwezeshwa kukutana na kusheherekea sikukuu ya Thanksgiving Marekani.

Wakimbizi kutoka kote duniani ambao wako eneo la Washington watakutana pamoja kusherehekea sikukuu ya kwanza ya kutoa shukrani, yaani Thanksgiving, nchini Marekani. 

Wakimbizi kutoka kote duniani ambao wako eneo la Washington watakutana pamoja kusherehekea sikukuu ya kwanza ya kutoa shukrani, yaani Thanksgiving, nchini Marekani.

Katika nchi mpya waliyopokelewa, Marekani, mamia ya wakimbizi kutoka sehemu zote duniani walikusanyika mapema mwezi Novemba kusherehekea Thanksgiving.

Hawa wakimbizi walisherehehekea kwa mara ya kwanza sikukuu hii.

Anila Karimzai, Mkimbizi wa Afghanistan anaeleza: “Kwa kuja hapa, najihisi vizuri na nina furaha kuwa na kila mtu, kuna watu wengine kutoka sehemu mbali mbali. Nina furaha kushiriki katika sherehe za Thanksgiving na watu wengi wanafuraha.”

Thanksgiving nchini Marekani inaadhimishwa kila mwaka katika Alhamisi ya nne ya mwezi Novemba.

Paredi iliyoandaliwa na kampuni ya Macy kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kutoa shukrani Thanksgiving Jumatano Novemba 23. 2022.
Paredi iliyoandaliwa na kampuni ya Macy kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kutoa shukrani Thanksgiving Jumatano Novemba 23. 2022.

Inasherehekewa kwa chakula ambacho ulikuwa ni utamaduni wa wakoloni wa Kiingereza na nchini Marekani na wazawa katika mia ya mwanzoni ya 1600.

Wamarekani wengi wanapika vyakula kama vile bata mzinga, viazi vitamu na mchuzi wakati wakiitumia sikukuu hii kuwa pamoja na marafiki na familia.

Kwa baadhi ya wakimbizi wa Aghanistan, kula bata mzinga kilikuwa kitu kipya.

Nazifa Karimzai, Mkimbizi wa Afghanistan: “Kwa hakika nafurahia. Chakula kizuri sana. Ni mara ya kwanza nimekula bata mzinga.”

Ili kuwafahamisha wageni na utamaduni wa Kimarekani, baraza la jamii la maendeleo la Waethiopia au ECDC. Hii ni moja ya taasisi za siku nyingi za makazi kwa wakimbizi nchini Marekani iliandaa hafla hiyo.

Tsehaye Teferra, wa ECDC anafafanua: “Kimsingi, tunashirikiana nao katika sikukuu muhimu za Marekani. Pia, tunajaribu kuzileta pamoja jamii ambazo ni wenyeji wa wakimbizi katika eneo ili waweze kula pamoja. Wanaweza kubadilishana mawazo. Wanaweza kubadilishana ushirikiano.”

Mina Tarin amekuwa nchini Marekani tangu Julai mwaka 2022. Anasema kwamba anashukuru kuwepo nchini Marekani baada ya kile ambacho amekipitia.

Mina Tarin, Mkimbizi wa Afghanistan alieleza: “Ningependa kumshukuru kila mtu hivi leo, hasa siku ya thanksgiving, kwa kuwasaidia wa Afghanistan kuondoka na madhila ambayo yanawakumba nchini Afghanistan hivi sasa.”

Maelfu ya wa Afghanistan wamekimbilia nchini Marekani baada ya Taliban kuchukua uongozi Agosti mwaka 2021, na wakimbizi wengi hapa wanasema wanashukuru kwa hilo.

((Khadija Riyami, VOA Washington))

XS
SM
MD
LG