Papa Francis wakati wa hafla hiyo ametoa wito mpya wa kuwasaidia wasiojiweza katika jamii, huku akikemea tabia za kujitafutia umaarufu zinazo funika kilio chao cha kuomba msaada. Ikiwa siku ya katoliki ya kuadhimisha siku ya masikini dunia, takriban watu maskini 1,300 walialikwa kwenye chakula hicho, wakati watoto wadogo wakipata nafasi ya kukaribia na kucheza na kiongozi huyo wa kidini.
Wakati wa misaa kabla ya kupata chakula, Papa Francis alikemea kutelekezwa kwa wakimbizi pamoja na watu maskini. Kiongozi huyo ameongeza kusema kwamba vita vya Ukraine vinaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa watu maskini ambao wanajikwamua kutoka kwenye athari za janga la corona pamoja na majanga megine kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.