Utawala wa kijeshi uliyochukua madaraka nchini Myanmar mapema mwaka jana umesema kwamba Malaysia imerejesha mamia ya raia wake kwa ndege za kukodisha katika miezi ya karibuni , ukiongeza kuwa wengi wao wanarejea bila hiari .
Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yanadai kwamba Malaysia inawalazimisha kurejea baada ya kukamatwa kwa kigezo cha kuwa nchini humo kinyume cha sheria.
Kuna hofu kwamba baadhi ya waomba hifadhi watakamatwa, kuteswa au hata kuuwawa baada ya kurejea Myanmar. Jeshi la taifa hilo linalaumiwa kwa kukamata na kuuwa maelfu ya raia wake, kama juhudi ya kunyamazisha wanaopinga utawala wake.