Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:45

Shirika la UN lawafukuza kazi wanao husishwa na shambulizi la kigaidi Israel


Wapalestina wakikusanyika kupokea magunia ya unga yanayo sambazwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya huduma huko Palestina (UNRWA), Rafah.
Wapalestina wakikusanyika kupokea magunia ya unga yanayo sambazwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya huduma huko Palestina (UNRWA), Rafah.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya huduma limewafukuza kazi wafanyakazi wake kadhaa kwa kuhusika na shambulizi la kigaidi la Oktober 7 lililofanywa na Hamas  dhidi ya Israel.

Israel

Israel imepongeza uamuzi wa nchi kadhaa, ikiwemo Marekani wa kusitisha ufadhili kwa shirika hilo. Wasi wasi ulitolewa juu ya jinsi utakavyoathiri wapalestina huko Gaza wanaojitahidi kutafuta chakula kutokana na kuendelea kwa vita.

Wakidai kuachiliwa kwa mateka, waandamanaji wa Israel walikusanyika tena Jumapili katika kivuko cha mpakani cha Kerem Shalom. Na kuzuia kwa muda misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Wapalestina

Wapalestina wamekuwa wakijitahidi kupata walau unga mdogo wa kujikimu, wakati Umoja wa Mataifa umeonya kuwa baadhi ya maeneo yanakabiliwa na njaa.

Mpalestina Asiyekuwa na Makazi aeleza: “Hii ni kwa ajili ya watu saba, ona ulivyo mdogo. Gharama yake ni shekel 50.” Hiyo ni sawa na dola 13 za Marekani.

UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi – UNRWA, linahusika na kuwasaidia takriban theluthi mbili ya watu milioni 2.3 huko Gaza, hivi sasa linakabiliwa na mzozo wake mwenyewe.

Wafanyakazi wake 12 wameshutumiwa kuhusika na shambulizi la kigaidi la Oktoba 7 lililofanywa na Hamas nchini Israel ambapo watu 1,200 waliuawa na takriban 240 walichukuliwa mateka.

Katibu Mkuu wa UN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amethibitisha Jumapili katika taarifa yake kwamba wengi walioshutumiwa wamefukuzwa kazi na uchunguzi unaendelea. Pia amezitaka walau nchi tisa, ikiwemo Marekani, kufikiria tena uamuzi wao wa kusitisha ufadhili kwa shirika hilo.

Wawakilishi wa kudumu kwa Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu – Arabu League katika kikao cha dharura mjini Cairo walijadili suala hilo.

Mohannad Aklouk, Mwakilishi wa Palestina katika Arab League: “Nchi ambazo zinawajibika kwa kuendelea kwa ufadhili wa UNRWA na siyo kufuata viwango viwili. Wasionyeshe majibu ya haraka sana.”

Balozi wa Israeli UN

Balozi wa Israel katika Umoja wa Mataifa Gilad Erdan ameonya jana Jumapili kwamba nchi ambazo zinaendelea ufadhili kwa UNRWA kabla ya uchunguzi wa kina kukamilika,, kwa maneno yake, “ni vyema zifahamu kuwa fedha zao huenda zilitumiwa kwa ugaidi.”

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu wakati huo huo amejaribu kutuliza maandamano ya ndani ya nchi kwa wale ambao wanataka afanye mengi zaidi kuhakikisha marekani wanarejea, na kuutaka uongozi wa Israel kujiuzulu.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel: “Hiyo inaimarisha tu madai ya Hamas, inaongeza madai yao na kutuweka mbali sana na lengo tunalolitaka – kurejea kwa mateka wote.”

Sitisho Jipya la Mapigano

Wakati Israel inaendelea kuwalenga wanamgambo wa Hamas huko Gaza, wawakilishi wa Qatar, Israel, Marekani na Misri walisemekana walikuwa katika mkutano jana Jumapili kufanya mashauriano na uwezekano wa sitisho jipya la mapigano na kuachiliwa kwa mateka zaidi.

Habari zimekuja wakati Wizara ya Afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas imetangaza kuwa idadi ya vifo vya raia huko imevuka elfu 26.

Ripoti ya mwandishi wa VOA Veronica Balderas Iglesias

Forum

XS
SM
MD
LG