Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:29

Mahakama ya UN yaiamuru Israel kuzuia mauaji ya kimbari...


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, mstari wa mbele, akiwa Johannesburg akisikiliza kesi ya
uamuzi wa mahakama ya juu ya UN, Jan. 26, 2024.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, mstari wa mbele, akiwa Johannesburg akisikiliza kesi ya uamuzi wa mahakama ya juu ya UN, Jan. 26, 2024.

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Kimataifa ya Haki imeiamuru Israel “kuchukua hatua zote katika uwezo wake” kuzuia mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Ukanda wa Gaza, lakini imesita kuiamuru kuhusu sitisho la mapigano katika eneo hilo lenye vita.

Uamuzi wa awali uliotolewa Ijumaa na jopo la majaji 17 wa ICJ iliiamuru Israel kuwezesha kipengele cha huduma za msingi na misaada ya kibinadamu huko Gaza, ambako eneo kubwa lenye takriban watu milioni 2.3 wanajitahidi kutafuta chakula na makazi baada ya miezi mitatu ya mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas.

Kesi ilifikishwa kwenye mahakama hiyo na Afrika Kusini, ambayo ilidai kwamba Israel inakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mwaka 1948 kuhusu Mauaji ya Kimbari, ambao ulipitishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia na mauaji ya Holocaust.

Katika kuwasilisha maamuzi yake, Jaji Joan Donoghue ambaye alisimamia katika kesi hiyo alisema kuzuia mauaji ya kimbari, kwa mujibu wa mkataba huo, itajumuisha , “kuzuia athari kubwa za kimwili au maumivu ya kiakili kwa wanachama wa kundi na kwa makusudi kufanya mambo kuhusu kulifanyia uharibifu kundi hilo.”

Donoghue amesema kama sehemu ya uamuzi Israel lazima ichukue hatua za haraka ili “ikiwezesha kipengele cha huduma za haraka za mahitaji ya msingi na misaada ya kibinadamu ili kushughulikia hali mbaya sana ya maisha.”

Israel imepuuza shutuma hizo za Afrika Kusini kuwa ni undumila kuwili na kuonyesha “dunia imegeuka juu chini.” Viongozi wa Israel walitetea mashambulizi yao ya anga na ardhi huko Gaza kama majibu halali kwa shambulizi la Hamas la Oktoba 7, wakati wanamgambo walipovamia jamii za Israel, na kuua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka watu 250.

Kufuatia uamuzi huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipinga madai ya mauaji ya kimbari ni ya “kukasirisha” na kuapa kuendelea na vita hivyo.

Maafisa wa Palestina kwa kiasi kikubwa wamepongeza uamuzi huo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imesema ilikuwa ni ukumbusho mzuri kwamba “hakuna taifa ambalo liko juu ya sheria.” Sami Abu Zuhri, afisa mwandamizi wa Hamas, aliiambia Reuters kuwa uamuzi huenda ukachangia ili “kutenga ukaliaji kimabavu na kuonyesha uhalifu wake huko Gaza.”

Kundi la utetezi la Human Rights Watch limepongeza uamuzi huo. Katika taarifa yake, mkurugenzi wa masuala ya haki ya kimataifa Balkees Jarrah, amesema kuwa uamuzi “unaiweka Israel na washirika wake katika kuangaziwa kuwa hatua za haraka zinahitaji kuchukuliwa kuzuia mauaji ya kimbari na ukatili zaidi dhidi ya Wapalestina huko Gaza.”

Jarrah amesema uamuzi wa “haraka” ni utambuzi wa hali mbaya huko Gaza.

Hatua za awali zilizotolewa na mahakama ya dunia zina nguvu ya kisheria, lakini haiko bayana kama Israel itaheshimu. Mahakama, wakati huo huo, ilitarajiwa kuchukua miaka kadhaa kutoa uamuzi kwa kesi kamili ya mauaji ya kimbari iliyofikishwa na Afrika Kusini.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG